Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wanawake kumulikwa Afghanistan

Rashida Manjoo,mtalaamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake.(Picha ya UM/maktaba)

Ukatili dhidi ya wanawake kumulikwa Afghanistan

Mtaalamu maalumwa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Rashida Manjoo, anataraji kufanya ziara nchini Jamhuri ya kiislamu ya Afghanistan kwa lengo la kutathimini hali ya ukatili dhidi ya kundi hilo ikiwamo vyanzo na madhara yake  nchini humo .

Akitangaza ziara yake hiyo inayoanza November nne hadi kumi mwaka huu Bi Manjoo amesema ukatili dhidi ya wanawake unasalia ukatili kinyume na haki za binadmau unaokuwa na kuathiri kila nchi duniani.

Mtaalamu maalum huyo ambaye katika  ziara yake atakutana na mamalaka za serikali na wawakilishi wa asasi za kiraia mjini Kabul, Herat na Jalalabad amesisistiza pia kuw akila nchi duniani ina jukumu la msingi la kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na kuongeza kuwa jukumu hilo hasa katika kuhakikisha utekelezaji wake linasalia kuwa la serikali.