Mzozo CAR waibua sintofahamu kwa wakulima CAR: Ripoti

30 Oktoba 2014

Uporaji mkubwa na ukosefu wa usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR umeleta sintofahamu katika hali ya mazao, mifugo na uvuvi.

Hiyo ni kulingana na ripoti mpya ya shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAO na lile la mpango wa chakula, WFP iliyobainisha kushuka kwa kiasi kikubwa kwa uzalishaji wa kilimo.

Ripoti imetaja sababu kuwa ni hali ya vurugu ya kidini nchini CAR tangu Desemba 2012, na kusababisha kusambaratika kwa maisha ya mamia ya maelfu ya watu.

Ikilinganishwa na viwango vya kabla ya mgogoro, FAO inasema inakadiriwa idadi ya mifugo kuwa chini kwa kiwango cha asilimia 77.

Afisa wa FAO Alessandro Costantino, alizuru mji mkuu wa CAR, Bangui hivi karibuni.

"Wakulima wanateseka kutokana na uporaji, uharibifu wa mazao na hifadhi na kilicho kibaya zaidi, wakulima wana hofu ya kwenda mashambani mwao."

FAO inatoa wito msaada wa ziada uongezwe katika uzalishaji wa chakula na sekta ya kilimo.

Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa wakulima wanaendeleza shughuli nyingine ya kupata mapato kama vile kuuza kuni na mkaa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter