Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya ukeketaji haipaswi kuonewa haya: Ban

Katibu mkuu wa UM Ban Ki-Moon alipokutana na mwanaharakati dhidi ya ukeketaji Fahma Mohammed nchini Uingereza mwezi Juni mwaka huu. (Picha: Eskinder Debebe)

Vita dhidi ya ukeketaji haipaswi kuonewa haya: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameshiriki uzinduzi wa kampeni ya vyombo vya habari dhidi ya ukeketaji, FGM huko Nairobi, Kenya akisema kitendo hicho hakipaswi kuonewa haya. Taarifa kamili na Assumpta Massoi

(Taarifa ya Assumpta)

Kampeni hiyo inahusisha ushiriki wa vyombo vya habari katika kuandika habari dhidi ya ukeketaji ambapo pia kutakuwepo na tuzo ya kila mwaka kwa mwandishi bora an chombo cha habari kilichoandaa taarifa zinazowezesha kutokomeza mila hiyo potofu.

Ban ametaka vyombo vya habari kutumia fursa hiyo akisema nchini Uingereza kampeni kama hiyo na ujasiri wa msichana Fahma Mohammed vimewezesha serikali kuahidi kuelimisha shule juu ya madhila ya kitendo hicho.

Kampeni inahusisha mipango miwili ambapo wa kwanza mshindi wake atapata mafunzo ya miezi miwili kwenye ofisi za gazeti la Guardian nchini Uingereza ambao ni moja wa wafadhili wa kampeni hiyo na ya pili itanufaisha vyombo vya habari vitano nchini Kenya kusaidia kampeni dhidi ya ukeketaji.