Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya dunia yaongeza dola Milioni 100 kukabiliana na Ebola

Picha: UNMIL Photo/Emmanuel Tobey

Benki ya dunia yaongeza dola Milioni 100 kukabiliana na Ebola

Benki ya dunia imetangaza nyongeza ya dola Milioni Mia Moja kwa ajili ya kukabiliana na Ebola huko Afrika Magharibi. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Kiwango hicho kitafanya mchango wa benki hiyo kwenye harakati dhidi ya Ebola kufikia dola Milioni 500. Mchango huu wa karibuni zaidi unalenga kuharakisha kasi ya kupelea wahudumu wa afya kwenye nchi tatu zilizokumbwa zaidi na Ebola ambazo ni Liberia, Guinea na Sierra Leone.

Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim amesema wahudumu hao wanahitajika ili kutibu wagonjwa wagonjwa wa Ebola, kuimarisha uwezo wa mfumo wa afya kwenye nchi hizo ikiwemo tiba dhidi ya magonjwa mengineyo.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takribani wahudumu wa afya wa kimataifa 5,000 wanahitajika kwenye miezi michache ijayo.