Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ustawi wa vijana hutegemea ushiriki wao katika utetezi wa sera: Mshiriki kutoka Tanzania

Vijana wakiwa makao makuu ya UM, wakati wa kongamano la vijana. Picha ya UM/Mark Garten.(maktaba)

Ustawi wa vijana hutegemea ushiriki wao katika utetezi wa sera: Mshiriki kutoka Tanzania

Vijana jitokezeni kutetea sera zenu kwa maslahi yenu. Ni kauli ya mmoja wa washiriki wa kongamano la vijana kuhusu sera linaloendelea jini Baku, Azerbaijan, Selemani Kitenge ambaye amezungumza katika mahojiano maalum na Basma Baghall wa idhaa ya kiarabu ya Umoja wa Mataifa.

Kitenge ambaye ni mwanaharakati wa vijana amesema kuna matumaini ya ustawi wa vijana kutokana na rasimu ya katiba nchini Tanzania inayotoa mwanya kwa vijana kuunda baraza lao. Kitenge anaanza kwa kueleza ushirikiwake kwenye mkutano.

(SAUTI MAHOJIANO)