Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa itoe usaidizi maalum kwa nchi zinzaoathriwa na mgogoro wa Syria: OCHA

John Ging, Mkuu wa operesheni ndani ya OCHA (Picha:UM/JC McIlwaine)

Jumuiya ya kimataifa itoe usaidizi maalum kwa nchi zinzaoathriwa na mgogoro wa Syria: OCHA

Licha ya michango kutoka kwa nchi wanachama katika kuwakwamua wananchi wa Syria ambao wanakumbana na madhila ya machafuko nchini humo, mshikamano zaidi  wa jumuiya ya kimataifa unahitajika katika kusaidia majirani wa nchi hii ambao wanatumia fedha nyingi kufuatia mgogoro huo kuvuka mipaka.

Hiyo ni kauli ya mkuu wa wa operesheni wa ofisi ya  Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu Ocha, John Ging  alipokutana na waandishi wa habri mjini New York kuzungumzia hali ya migogoro huko Mashariki ya kati.

Ging amesema ni lazima kuwe na usaidizi maalum mbali na fedha za kusaidia hali za kibinadamu ambazo amesisitiza zinahitajika zaidi

(SAUTI GING)

"Hayakuwa majukumu yao waliamua tu kutimiza kwa kufungua mipaka ya nchi zao kuruhusu watu kuingia kwa usalama wao lakini huu ni wajibu ambao  lazima jumuiya ya kimatifa isaidie katika fedha. Kwa sasa Lebanon. Uturuki na Jordan wamefikia kiwango cha mwisho cha uwezo wao na wana wajibu wa kusaidia idadi ya watu kwa hiyo lazima tufanye kitu kuwawezesha kuendelea kufungua mipaka."

Kuhusu Iraq amesema nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa rasilimali lakini hainufaiki na rasilimali hizo  inahitaji kusaidiwa kutokana na machafuko hasa wakati huu ambapo amesema majira ya baridi yanakaribia na hivyo kuongeza madhila kwa raia ambao wengi ni wakimbizi wa ndani na nje ya nchi .