Ban azuru Daadab, akutana na pia na Rais Kenyatta

29 Oktoba 2014

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametembelea kambi ya Daadab nchini Kenya ambayo inahifadhi maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia.Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephan Dujarric amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari.(Sauti ya Dujarric)

“Ametembelea hospitali iliyopo kambini hapo ikiwemo wadi ya wajawazito na kituo cha kuimarisha lishe, halikadhalika amekutana na wakimbizi pamoja na jamii zinazowahifadhi.”

Kwa mujibu wa msemaji huyo, baada ya kutembelea Daadab, Ban amekuwa na mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini Nairobi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter