Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagonjwa zaidi wa homa ya mafua ya ndege H7N9 wabainika China

Ufugaji wa kuku/Picha ya UM

Wagonjwa zaidi wa homa ya mafua ya ndege H7N9 wabainika China

Shirika la afya duniani, WHO limesema wagonjwa wengine wawili walioambukizwa kirusi cha homa ya mafua ya ndege, H7N9 wamethibitishwa nchini China.

WHO imesema imepokea taarifa kutoka kamisheni ya taifa ya afya na uzazi wa mpango nchini humo inayosema mmoja wa wagonjwa hao ana umri wa miaka Saba na anatoka kitongoji kimoja cha mji mkuu wa China, Beijing ilhali mwingine anatoka jimbo la Uyghur.

Hata hivyo tayari serikali ya China imechukua hatua ikiwemo kuimarisha ufuatiliaji, udhibiti na tiba dhidi ya ugonjwa huo ambapo mmoja wao yasemakana amekuwa anahusika na ufugaji wa kuku.

WHO imependekeza hatua kadhaa ikiwemo wasafiri kutoka nchi zenye mlipuko kuepuka mashamba yanayofuga kuku au masoko yanayouza ndege hao.

Hata hivyo haipendekezi vizuizi vya biashara dhidi ya nchi zenye ugonjwa huo wa homa ya mafua ya ndege au uchunguzi wa kina kwenye vituo vya kuingilia wasafiri kama vile viwanja vya ndege.