Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya vijana milioni 80 Asia hawana ajira UN

Picha: ESCAP

Zaidi ya vijana milioni 80 Asia hawana ajira UN

Zaidi ya watu milioni 80 ambao ni vijana walioko kwenye umri wa kuajiriwa katika eneo la Asia-Pacific wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira huku kukiwa na taarifa kwamba katika baadhi ya nchi hali ni mbaya zaidi kiasi.

Inasemekana kuwa katika baadhi ya nchi kiwango cha vijana hao kukosa ajira kimepindukia kikifikia zaidi ya mara saba jambo ambalo linaweza kuzusha hali ya hatari hapo baadaye.

Kwa kutambua hali hiyo, Umoja wa Mataifa uliwakutanisha zaidi ya vijana 300 katika kongamano maalumu lililofanyika Bangkok kwa ajili ya kujadiliana njia bora za kukwamua tatizo hilo. Vijana hao ni kutoka sekta mbalimbali na kwamba wamejadiliana kwa kina hatua zinazopaswa kufuatwa ili kuondoa tatizo hilo.