Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba viondolewe:Umoja wa Mataifa

Picha ya UM/Maktaba

Vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba viondolewe:Umoja wa Mataifa

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne limepitisha azimio linalotakna Marekani kuondoa vikwazo vya kibiashara na kifedha dhidi ya Cuba, vikwazo ambavyo vimekuwepo tangu mwaka 1960.

Nchi 188 kati ya 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa walipiga kura na kuunga mkono azimio hilo huku Marekani, Israel zikipinga ilhali Palau, Micronesia na visiwa vya Marshall havikupiga kura yoyote.

Kwa mujibu wa Brundo Rodriguez Parilla, mwakilishi wa kudumu wa Cuba kwenye Umoja wa Mataifa, vikwazo hivyo vimesababisha athari za kiuchumi zinazofikia thamani ya dola Trilioni Moja.

Hii ni mara ya 23 azimio la aina hiyo linapitishwa la kutaka vikwazo hivyo viondolewe.