Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malala akabidhi zawadi yake ya dola Elfu 50 kwa UNRWA

Malala asema atatoa tuzo lake kwa ajili ya kukarabati shule iliyoharibiwa.(Picha ya UNRWA)

Malala akabidhi zawadi yake ya dola Elfu 50 kwa UNRWA

Mwanaharakati Malala Yousfzai kutoka Pakistani ambaye ameshinda tuzo ya dunia ya mtoto amekabidhi zawadi yake ya dola Elfu Hamsini kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA.

Malala ambaye ni mtoto mwenye umri wa miaka 17 anayetetea haki ya elimu kwa watoto wote, amesema fedha hizo zitasaidia kujenga shule 60 zilizoharibiwa wakati wa mashambulizi ya hivi karibuni Ukanda wa Gaza.

Katika hotuba yake baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo nchini Sweden, Malala amesema mahitaji ni mengi kwani zaidi ya nusu ya wakazi wa Gaza ni wana umri wa chini ya miaka 18.

Amesema watoto hao wanahitaji elimu bora, matumaini n ahata fursa sahihi ili wajenge mustakhabali wao.

Malala ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya Amani ya Nobel, amesema bila elimu hakutakuwepo na Amani kwa hiyo ni vyema kushirikiana kuimarisha elimu.

Naye Kamishna Mkuu wa UNRWA Pierre Krähenbühl ameshukuru msaada huo akisema ni ishara ya jinsi Malala anavyotambua umuhimu wa mtoto kupata elimu.