Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yapewa tuzo kwa kuendeleza wanawake kiteknolojia.

Picha ya UNESCO/CC BY SA Eric Muthoga

Mashirika ya UM yapewa tuzo kwa kuendeleza wanawake kiteknolojia.

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa: lile la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, na shirika la wanawake UN Women, ni miongoni mwa taasisi zilizopewa tuzo za kutambua mchango wa kuendeleza maisha ya wanawake kupitia teknolojia katika mkutano unaoratibiwa na Shirika la kimataifa la mawasiliano ITU unaofanyika nchini Korea Kusini.Katika mahojiano na idhaa hii kutoka Korea Kusini Mkuu wa mawasiliano  katika mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, Innocent Mungy  anaeleza umuhimu wa tuzo hizo.

(SAUTI MUNGY)

Kadhalika Bwana Mungy amezungumzia mafanikio kwa  Tanzania Kenya na Uganda kuingia katika baraza la utawala la ITU.

(SAUTI MUNGY)