Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana jitokezeni kujadili mambo yenu: Mshiriki kutoka Tanzania

Selemani Y Kitenge, mwakilishi wa ujumbe wa Tanzania kwenye kongamano la kimataifa kuhusu sera za vijana. (Picha:UN/Basma Baghall)

Vijana jitokezeni kujadili mambo yenu: Mshiriki kutoka Tanzania

Wakati kongamano la vijana kuhusu sera likiendelea mjini Baku, Azerbaijan, mmoja wa washiriki kutoka Tanzania, amesema baadhi ya sera ni nzuri lakini tatizo ni vijana wenyewe.Selemani Kitenge amesema hayo alipohojiwa na Radio ya Umoja wa mataifa huko Baku.

(Sauti ya Selemani)

Bwana Kitenge akaulizwa ujumbe aliotoa kwenye kongamano hilo.

(Sauti ya Selemani)

Hata hivyo amesema nchini Tanzania kuna matumaini kutokana na katiba mpya iliyopendekezwa akisema ina kipengele kinachotoa fursa ya kuanzisha baraza la vijana, na hilo baraza litafanyia kazi mapendekezo ya vijana.