Mahitaji ya ajira Ulaya hayaendani na sifa walizo nazo vijana: ILO

29 Oktoba 2014

Utafiti mpya wa mpya ya shirika la kazi duniani, ILO imeonyesha ukosefu mkubwa wa uwiano kati ya stadi za kazi walizo nazo vijana huko barani Ulaya na mahitaji ya ajira kwenye soko. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Utafiti huo umeonyesha kuwa kati ya asilimia 25 na 45 ya wafanyakazi barani huko wana sifa za kupindukia kwenye ajira au hawana sifa za kutosha kuweza kuajiriwa jambo linalosababisha ukosefu huo wa uwiano kati ya ajira zinazotakiwa na stadi walizo nazo.

Mathalani nchini Ureno, moja ya nchi 24 zilizoguswa na utafiti huo, asilimia 50 ya wafanyakazi wako kwenye kundi hilo lisiloweza kuajiriwa popote.

Mchumi mwandamizi na mtakwimu kutoka ILO Theo

Sparreboom anaelezea walichobaini.

(Sauti ya Theo)

"Tunachofahamu juu ya tofauti hiyo kati ya mahitaji ya ajira na kilichopo ni udhaifu wa mawasiliano kati ya soko la ajira na mfumo wa elimu na pia tunafahamu hali hiyo inaongeza gharama sana kwa mtu binafsi, kampuni na jamii kwa ujumla. Lakini kile ambacho hatuna sasa hivi ni mfumo uliokubaliwa wa wa kupima tofauti hiyo."

Utafiti unaonyesha kuongezeka kwa kiwango cha walio na sifa za kupindukia hadi kushindwa kupata ajira kuliko wale wasio na sifa.

(Sauti ya Theo)

“Sababu ni  ongezeko kubwa la wafanyakazi vijana kwenye ajira zisizokidhi viwango.  Yaani wanaweza  kuajiriwa kirahisi kama vibarua kwa kuwa huko ni vigumu sana kupata ajira inayoendana na sifa alizonazo mwajiriwa.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter