Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni dhidi ya Ebola yapamba moto Sierra Leone

Ebola Sierra Leone. Picha: UNICEF/NYHQ2014-1586/BINDRA

Kampeni dhidi ya Ebola yapamba moto Sierra Leone

Nchini Sierra Leone, janga la Ebola linazidi kuenea kila uchao, jumuiya ya kimataifa inahaha kudhibiti na hatimaye kutokomeza janga hili wakati huu ambapo zaidi ya watu 4500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo wengi wao wakiwa ni huko Liberia, Guinea na Sierra Leone.

Kazi kubwa sasa ni kampeni ya kinga kwa wananchi ili kudhibiti maambukizi mapya, kazi ambayo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF imeanza huko Sierra Leone kama anavyosimulia Assumpta Massoi.