Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Janga la vipaumbele ndio tatizo kuu duniani: de Zayas

UN Photo/Amanda Voisard
Alfred De Zayas, Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu uendelezaji wa utaratibu wa kimataifa wenye uwiano na demokrasia. Picha:

Janga la vipaumbele ndio tatizo kuu duniani: de Zayas

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu uendelezaji wa utaratibu wa kimataifa wenye uwiano na demokrasia Alfred De Zayas amesema kushindwa kwa nchi kutambua vipaumbele ndio chanzo cha kukata huduma za msingi kama vile afya na elimu kwenye bajeti huku zile za kijeshi zikitunishwa.

Akinukuu ripoti yake, de Zayas amewaeleza waandishi wa habari mjini New York, kuwa mwaka jana pekee serikali duniani zilitumia zaidi ya dola Trilioni Moja na Nusu kwa ajili ya shughuli za kijeshi akisema hata asilimia Kumi tu ingalitosha kwa malengo ya milenia na yale ya baada ya mwaka 2015.

(Sauti ya de Zayas)

“Kupunguza ukali wa bajeti hutumiwa kukata bajeti ya elimu, huduma ya afya na haitumiki kwa ajili ya kukata manunuzi au silaha au kupunguza ukubwa wa majeshi au vituo vya kijeshi na kadha wa kadha. Kwa hiyo ninachomba ni mabadiliko ya mtazamo.”

Bwana de Zayas amesema uendelezaji wa haki za binadamu utawezekana iwapo bajeti itaelekezwa kwenye huduma za afya ili kuhakikisha watu wanapata haki zao za msingi ikiwemo afya na elimu