Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yapongeza Uswisi kukubali majaribio ya chanjo dhidi ya Ebola

Dawa za kukabiliana na Ebola.Picha ya WHO/M. Missioneiro

WHO yapongeza Uswisi kukubali majaribio ya chanjo dhidi ya Ebola

Wakati harakati za kudhibiti Ebola zikiendelea, Shirika la Afya Duniani, WHO limekaribisha idhinisho lilotolewa na mamlaka ya Uswisi ya kudhibiti bidhaa za matibabu, Swissmedic, la kufanyia majaribio chanjo ya Ebola katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Lausanne.  Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Idhinisho hilo lina maana kwamba, chanjo inaweza kutumika kwa watu binafsi 120 katika mji wa Lausanne.

WHO imesema huu ni mwanzo wa hatua ya kuleta chanjo salama ya Ebola kwa ajili ya upimaji wa haraka.

Majaribio hayo ambayo yamepokea msaada kutoka kwa WHO, ni mfululizo wa hatua za hivi karibuni zinazoendelea kwingineko nchini Mali, Uingereza, na Marekani. Tarik Jasarevic ni msemajia wa WHO

(SAUTI Tarik Jasarevic)

Chanjo hii bado haijathibitishwa kuwa salama, na itafanyiwa majaribio watu watakaojitolea na ambao wana afya. Hii sio chanjo ya kuwapa kinga watu watakaokwenda Afrika Magharibi. Lakini iwapo miongoni mwa wanaojitolea, kuna wale watakaopelekwa kule, basi watapewa kipaumbele

Wakati huo huo, shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema  ujenzi wa meaeneo mawili ya matibabu ya Ebola kati ya manne umekamilika mjini Monrovia, Liberi