Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lamulika wanawake, Amani na usalama

UN Photo/Kay Muldoon
Picha:

Baraza la Usalama lamulika wanawake, Amani na usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu wanawake, Amani na usalama likiangazia madhila wanayopata wakati wa migogoro. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Mjadala ulimulika wanawake na wasichana wahanga wa mizozo inayosababisha wabakie wakimbizi ndani na nje ya nchi zao bila kusahau nafasi yao kwenye utatuzi wa migogoro.

Ujumbe wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon  ulisomwa na Mkuu wa UN-Women, Phumzile MlamboNgucka ukieleza wasiwasi wake juu ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana..

“Ninachukizwa na mashambulio dhidi ya wanawake na wasichana na ukiukwaji wa haki zao na hata watetezi wa haki zao. Natoa wito hatua zichukuliwe dhidi  ya ukwepaji sheria kwa wanaofanya vitendo hivyo.”

Mwingine aliyehutubia ni Naibu Mkuu wa masuala ya operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Edmond Mulet  akatoa pendekezo.

(Sauti ya Mulet)

“Lazima tutambue kuwa njia bora zaidi ya kulinda na kusaidia wanawake wakimbizi wa ndani ni kuwawawezesha wajisaidie wenyewe kwa kuwapa fursa ya kuamua pamoja na rasilimali za kiuchumi na kijamii na kuwawezesha".