Jukwaa la sera kuhusu vijana lafunguliwa Baku, Azerbaijan

28 Oktoba 2014

Kongamano la kwanza la kimataifa linalomulika sera kuhusu vijana limeanza rasmi leo mjini Baku, Azerbaijan, likileta pamoja watu 700 wapatao, wakiwemo watunga sera, mashirika ya kiraia, wasomi, watetezi wa masuala ya vijana, wabunge na wawakilishi mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Jukwaa hilo litatoa fursa kwa washiriki kutathmini hali ya sera kuhusiana na vijana, ikiwa ni miaka 20 tangu kuridhiwa kwa Mpango wa kimataifa wa kuchukua hatua kwa ajili ya vijana, mwaka 1995.

Katibu Mkuu Ban Ki-moon ametoa ujumbe huu wakati wa ufunguzi

Vijana ni viongozi wa kesho, lakini tunapaswa kuwasikiliza vyema leo. Vijana wanapoongea na kutambua sera zenye umuhimu kwao, serikali, biashara na jamii kwa jumla zinaweza kunufaika”

Mjumbe wa Katibu Mkuu kuhusu vijana, Ahmed Alendawi, akasisitiza ujumbe wa kuwekeza kwa vijana..

Kauli mbiu ya kuadhimisha miaka ishirini ya mpango wa kimataifa kwa vijana ni, “Wekeza kwa Vijana”. Ni kwa sababu vijana hawaombi usaidizi, lakini wanaomba uwekezaji

Jukwaa hilo litakalohitimishwa mnamo Oktoba 30, limeandaliwa na Ofisi ya Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Shirika la Mpango wa Maendeleo, UNDP, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na wadau wengine, likifadhiliwa na serikali ya Azerbaijan.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter