Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yazungumzia vurugu baina ya wakimbizi Sudan Kusini

Wakimbizi wa Sudan Kusini.Picha ya UM/JC Mcllwaine

UNMISS yazungumzia vurugu baina ya wakimbizi Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini,  UNMISS umesema uchunguzi unaendelea baada ya tukio la jumapili la mashambuliano kati ya vikundi viwili kwenye kituo cha kuhifadhi wakimbizi wa ndani nje kidogo ya mji mkuu Juba.

Msemaji wa UNMISS Joseph Contreras amesema kwa sasa majeruhi 20 kati ya 60 wamelazwa ambapo Wanne kati yao hali zao ni mbaya.

Amesema mabomu ya kutoa machozi yalirushwa ili kutenganisha makundi hayo ambapo walinda amani wawili kutoka Nepali walijeruhiwa kidogo.

(Sauti ya Contreras)

Watuhumiwa wawili wanashikiliwa katika kizuizi cha UNMISS na taratibu zinaendelea ili wakabidhiwe kwa mamlaka husika kwa ajili ya uchunguzi na kufunguliwa mashtaka.”

UNMISS imetoa wito kwa viongozi wa kijamii kwenye vituo hivyo vya kuhifadhi wakimbizi wa ndani kushughulikia suala la uhalifu.