Haki ya uhai nchini Iran yamtia hofu mtaalamu wa haki za binadamu

28 Oktoba 2014

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Iran, Ahmed Shaheed amesema haki ya uhai nchini humo bado inamtia wasiwasi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, kabla ya kuwasilisha ripoti yake kwa Kamati ya Tatu ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa hii leo, Jumanne, Shaheed amesema kuanzia mwezi Juni mwaka jana watu 852 wameuawa wakiwemo watoto wanane.

Amesema kinachotia hofu zaidi ni makosa wanayoadhibiwa nayo ikiwemo mengine ya kisiasa na hata umri wa wao ikiwemo watoto.

Mtaalamu huyo akagusia pia kuuawa kwa mwanamke mmoja nchini Iran Jumamosi iliyopita.

(Sauti ya Shaheed)

“Nilishtushwa sana na kuuawa kwa Rehani Jabari mwishoni mwa wiki. Katika mawasiliano kadhaa na serikali ya Iran nilikuwa nahoji mambo kadhaa kuhusu hukumu hiyo na hadi sasa sijapokea majibu ya kutosha juu ya msingi wa hukumu ile, hususan haki yake wakati kesi inasikilizwa. Na  bila shaka kamishna mkuu wa haki za binadamu aliibua shaka dhidi ya kesi hiyo, halikadhalika taasisi nyingine za haki za binadamu.”

Kwa mujibu wa Shaheed, ripoti hiyo ilizingatia taarifa alizokusanya kutoka vyanzo rasmi mbali mbali ikiwemo tovuti za bunge, ripoti za serikali ya Iran kwa Umoja wa Mataifa na nyingine alizopokea kutoka mashirika ya haki za binad

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter