Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma ya afya kwa wakaazi wa Kismayo. Somalia yaleta afueni:

UN Photo/Ramadan Mohamed Hassan
Kliniki inayoendeshwa na AMISOM, Kismayo, Somalia. Picha:

Huduma ya afya kwa wakaazi wa Kismayo. Somalia yaleta afueni:

Wakati nchi ya Somalia ikiendelea kujikwamua kutokana na minyororo ya vita kwa wenyewe kwa wenyewe iliyokuwa imeifunga nchi hiyo kwa zaidi ya miongo miwili, wananchi kwa muda mrefu  wamekabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo upatikanaji wa huduma muhimu kama vile za afya.

Lakini sasa kuna nuru gizani kufuatia mradi unaondeshwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNSOM  kwa ushirikiano na walinda amani kutoka Umoja wa Afrika, AMISOM ambao wanatoa huduma ya afya  kwa wakaazi wa mji wa Kismayo nchini humo,

Je ni kwa kiasi gani, na afueni ni ipi? basi ungana na Grace Kaneiya katika makala ifuatayo