Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majira ya baridi yakikaribia hali ya watu waliofurushwa makwao yazorota: UNHCR

Majira ya baridi yakikaribia hali ya watu waliofurushwa makwao yazorota: UNHCR

Huku mzozo wa Ukraine ukiingia msimu wake wa kwanza wa baridi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Wakimbizi, UNHCR, liko mbioni kuwasaidia baadhi ya watu wanoishi katika mazingira magumu ya kimakazi ili waweze kukabiliana na baridi kali inayotarajiwa.

Taarifa ya UNHCR inasema mgogoro unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo umechangia kuvuinjika kwa huduma za msingi na hivyo kusukuma watu zaidi kukosa makazi .

Mahitaji ya msaada wa kibinadamu yanazidi kuongezeka, hususan karibu na mji wa Donetsk, Kharkiv, Kyiv, na katika maeneo ya Dnipropetrovsk na Zaporizhzia.

UNHCR imesema katika taarifa kwamba idadi ya watu waliokimbia makwao Ukraine imeongezeka na kufikia watu 430,000, huu ukiwa ni ongezeko la watu 170,000 zaidi ya mwanzoni mwa Septemba.