Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano na Dk Pamphil Silayo-UNICEF kuhusu uhai wa watoto

Mtoto na mama yake. Picha ya UNICEF

Mahojiano na Dk Pamphil Silayo-UNICEF kuhusu uhai wa watoto

Tanzania imetimiza lengo la maendeleo ya milenia namba nne linaloangazia uhai wa watoto ikiwa bado ukomo wa malengo hayo haujafikiwa mwakani 2015.

Hatua hii imewezeshwa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau ikiwamo serikali ya nchi hiyo ambapo utolewaji wa chanjo umekuwa siri kubwa ya mafaniko.

Katika mahojiano na  Joseph Msami wa idhaa hii mtaalamu wa chanjo wa UNICEF Tanzania Dk Pamphil Silayo  anasema kutoa kipaumbele kwa afya ya watoto pamoja na utayari wa wahudumu wa afya ni moja ya fursa muhimu. Kwanza Dk Silayo  anaanza kwa kueleza haua hiyo ilivyofikiwa.