Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa Ebola una athari kwa upatikanaji wa chakula kwa miezi ijayo:Ripoti

Picha: WFP/Merel van Egdom

Ugonjwa wa Ebola una athari kwa upatikanaji wa chakula kwa miezi ijayo:Ripoti

Wakati dunia ikiendelea kukabiliana na mlipuko wa Ebola Shirika la chakula na kilimo duniani FAO  na Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kwa ushirikiano na serikali ya Liberia wametoa ripoti kuhusu usalama wa chakula nchini humo.

Takwimu kufuatia utafiti huo zinaonyesha upungufu wa mazao kabla na baada ya mavuno, kusambaratika kwa soko, mfumko wa bei ya bidhaa muhimu na changamoto za kufikia maeneo ya vijijini kwa ajili ya miundo mbinu duni.

Makadirio hayo yanaonyesha kwamba kuenea kwa Ebola kumeathiri usalama wa chakula katika nchi za Guinea, Sierra Leone naLiberia na bei za vyakula zinasuasua. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP mjini Geneva.

“Mlipuko wa Ebola ukiendelea kwa muda wa miezi minne au mitano, wakati wakulima wanaanza kutayarisha ardhi, tuna wasiwasi kubwa kuhusu msimu wa upandanji wa mimea na mavuno ya mwaka 2015. Ugonjwa huo huenda ukaathiri mavuno.”