Kisa cha kwanza cha Ebola chagundulika Mali

24 Oktoba 2014

Wakati ugonjwa wa Ebola ukiendelea kushuhudiwa Afrika Magharibi Shirika la afya duniani limetoa ripoti kuhusu kisa cha ebola nchini Mali kufuatia kugunduliwa kwa mtoto wa miaka miwili ambaye alisafiri kuenda nchi jirani ya Guinea ambako aliambukizwa ugonjwa huo.Mali ni nchi ya sita Afrika Magharibi kuwa hatarini ya ugonjwa  huo. Wataalam wa WHO wamekuwa nchini Mali huku Shirika hilo likitarajia kutuma wataalam wengine wanne katika siku zijazo ili kutathmini uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.

Fadela Chaib ni msemaji wa WHO

"Sasa tunachojua ni kwamba watu 43 wamebainiwa kama watu waliokaribia mtoto huyu wa kike. Hivi wanafuatiliwa. Miongoni mwao kuna wauguzi 10. Hatua zimeshachukuliwa na mamlaka za Mali. Wamesafisha kituo cha afya ambapo mtoto alipelekwa na wameanza kufanyakazi na WHO. Bahati nzuri tulikuwa na timu yetu ya watu wa tatu nchini humo tangu oktoba 19, waliopelekwa kufanyakazi na serikali ya Mali katika maandalizi ya kupambana na Ebola kwa nchi 15 zinazoopakana na  Guinea, Sierra Leone na Liberia. "

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter