Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polio inaweza kutokomezwa, lakini bado kuna changamoto- UNICEF

Polio inaweza kutokomezwa, lakini bado kuna changamoto- UNICEF

Mwashauri Mkuu, na kiongozi wa timu ya kukabiliana na polio katika shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, Peter Crowley amesema  hatua kubwa zimepigwa katika kutokomeza ugonjwa wa kupooza, au Polio, duniani japo kuna changamoto.

Crowly amesema kampeni ya miaka 26 ya kujaribu kutokomeza Polio imefanikiwa katika kupunguza kupooza na kufa kwa watoto zaidi ya milioni 11, na kwamba sasa katika mataifa 190 hakuna hofu ya kuambukizwa polio.

Sauti ya Crowly

“Tumekaribia. Tuko karibu  sana. Asilimia 99.9 ya polio imetokomezwa duniani. Visa  vya kila mwaka vya polio vimepungua kutoka  350 000 mwaka wa 1988 hadi 416 mwaka wa 2013. Na mwaka huu ni 243.”

Lakini Crowly ameonya

 “Wakati tunaposherehekea mafanikio haya, hatupuuzi changamoto zilizosalia. Utokomezaji si rahisi; kwani imewahi kufanywa wakati mmoja awali na ndui. Na hatua ya mwisho hua ngumu ikizingatiwa mahali ambapo kirusi kimejificha”

Kuhusu juhudi za bara la Afrika za kupambana na Polio, Mkurugenzi wa Utokomezaji wa Polio katika taasisi ya Bill and Melinda Gates, Jay Wenger amesema

Sauti Jay Wenger

 “Tukiwa na jumla ya visa 22, vilivyoripotiwa barani Afrika mwaka huu, tuko njiani kutokomeza polio Afrika ifikiapo mwaka 2015.”

Siku ya Polio Duniani inaadhimishwa kila mwaka tarehe 24 Oktoba.