Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio bungeni Canada lashtusha IPU

Martin Chugong, Katibu Mkuu wa IPU. (Picha:UN/Zach Krahmer)

Shambulio bungeni Canada lashtusha IPU

Umoja wa mabunge duniani, IPU umeshtushwa na taarifa za mashambulizi kwenye jengo la bunge la Canada siku ya Alhamisi na kusema kitendo hicho ni shambulio dhidi ya demokrasia.

Taarifa ya IPU imemkariri Katibu Mkuu wa IPU Martin Chungong akieleza masikitiko yake na huzuni akisema shambulio hilo dhidi ya taasisi inayowakilisha utashi wa wananchi haliwezi kuhalalishwa kwa misingi yoyote ile.

Bwana Chugong ameeleza mshikamano wa IPU na wananchi wa Canada na wawakilishi wao katika kipindi hiki kigumu.

Katika tukio hilo iliripotiwa kuwa askari mmoja aliuawa wakati akiwa lindoni kwenye jengo la makumbusho ya taifa ya vita lililo karibu na bunge la nchi hiyo.