Mafuriko yaathiri maisha ya wakimbizi Kenya
Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR nchini Kenya linafanya kila liwezekanalo kunusuru maisha ya wakimbizi kutokana na mafuriko katika kambi za Kakuma na Daadab nchini humo.
Afisa wa UNHCR nchini humo Emanuel Nyabera ameiambia idhaa hii kuwa mafuriko hayo yamesababisha kifo cha mtu mmoja katika kambi ya Kakuma na kwakuwa amsimu wa mvua unaendela UNHCR inahakikisha usalama wa wakimbizi katika kambi hizo ikiwa ni pamoja na kudhibiti magonjwa ya milipuko yatokanayo na mafuriko.
(SAUTI NYABERA)
Akizungumzia hatua zinazochukuliwa na UNHCR katika kujihami dhidi ya mafuriko nchini Burundi mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini humo Abel Mbilinyi anasema
(SAUTI MBILINYI)