Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mji mkongwe Zanzibar hatarini kutoweka, UNESCO kuunusuru

UN Photo/Milton Grant
Picha:

Mji mkongwe Zanzibar hatarini kutoweka, UNESCO kuunusuru

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO limesema juhudi za makusudi zinahitajika ili kuunusuru mji mkongwe wa Zanzibar ambao umeingia katika orodha hatarishi ya kutoweka katika urithi wa dunia.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa hii afisa wa UNESCO Tanzania Moshi Kiminzi amesema shirika hilo linachofanya kwa sasa ni kuwasiliana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, ya Muungano pamoja na mamlaka ya mji mkongwe kuhakikisha eneo hilo muhimu katika historia ya Afrika Mashariki linarejeshewa hadhi yake stahiki.

(SAUTI MAHOJIANO)