Ushahidi wa kisayansi mwarobaini wa kuwadhibiti wahalifu wa kibinadamu-UM

22 Oktoba 2014

Ushahidi wa kimazingira unaokusanywa na kufanyiwa uchunguzi kwenye maeneo ulikofanyika uhalifu unaweza kutumikakamanjia ya kukabiliana na wale wanaokwepa kuwajibishwa kwa kufanya vitendo vya utesaji. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

Hayo ni kwa mujibu wa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya vitendo vya unyanyasaji na mateso Juan E Mendez ambaye amesisitiza kuwa wahusika wa matukio ya uhalifu wanapaswa kuadhibiwa bila kujali kinga waliyonayo.

Mtaalamu huyo maesema kuwa kuna njia nyingi za kuweza kuwabana watuhumiwa hao ikiwamo utumiaji wa ripoti za kitabibu ambazo zinatoa matokeo ya kisayansi juu ya wale walioathirika na matukio ya uonevu.

Hata hivyo amesema kuwa ili hili lifanikiwa lazima kuwe na ushirikiano baina ya waaathirika, vyombo vya dola na tasisi za kitaaluma hatua ambayo itaiwezesha mahama kuwa uwigo mpana wa kuamua mashauri

"Ujuzi wa kisayansi hasa zaidi ushahidi wa kidaktari ni hatua muhimu itazozifanya dola zichukua jukumu la kukomesha ukatili. Moja ya majukumu hayo ni kuchunguza, kuendesha kesi na kuadhibu kwa kila jambo liwe la kikatili, utesaji ama kudhihaki.Na kwa kweli siyo kwamba hili halijafanywa kwa vile hakuna ushahidi wa kutosha bali hakuna jitihada kubainisha vitendo hivyo hasa pale sayansi ya mabo haya yanapatikana."

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa pia amesisitiza haja ya wataalamu wanaohusika na mambo hayo kuachwa wakiendesha kazi zao katika mazingira ya uhuru.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter