Baraza la usalama lajadili hali ya amani Sudani Kusini

22 Oktoba 2014

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limejadili hali nchini Sudani Kusini ambapo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, Ellen Margrethe Løj,  amehutubia kikao hicho.  Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Mwakilishi huyo maalum wa Katibu Mkuu amesema hali ya amani nchini Sudani Kusini bado ni tete na hivyo akashauri.

(SAUTI ELLEN)

“Hakuna suluhu mbadala, ni lazima kuweka silaha chini na bila kuchelewa kutekeleza mkataba wa amani ili kuirejesah amani ya nchi kama awali. Huu ndiyo ujume ambao nimekuwa nikiutoa kwa  Watu wa Sudani Kusini, rais Kiir pamoja na kiongozi wa upinzani Dk Machar.”  

Kwa upande wake Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono kwenye mizozo, Zainab Hawa Bangura ambaye alihutubia baraza hilo kwa njia ya video kutoka Geneva amesema ziara yake ya hivi karibuni hivi nchini Sudani Kusini imemsikitisha hususani haki za wanawake na watoto .

(SAUTI BANGURA)

“Nchini kote wanawake wanaishi katika mazingira mabaya, hawana huduma za afya,hawana fursa za kutosha za kupata kipato chao na cha familia. Mawazo yao hayashirikishwi kwenye serikali na hata maamuzi mengine muhimu. Mwanaharakati mmoja aliniambia na hapa namnukuu, tunaishi katika utawala wa wanaume na sio wa kisheria.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter