Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi kame zatengewa Euro milioni 41

Maeneo kame.(Picha ya FAO)

Nchi kame zatengewa Euro milioni 41

Mpango wa miaka mitano utakaogharimu kiasi cha Euro milioni 41 kwa ajili ya kuwapiga jeki wakulima walioko katika maeneo yenye ukame umezinduliwa leo na inatazamiwa kwamba hatua hiyo itasaidia kukabiliana na kitosho cha ukosefu wa chakula.

Mpango huo ambao umezinduliwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya Umoja wa Ulaya, Shirika la Chakula na Kilimo FAO unalenga kuzinufaisha nchi za Afrika na zile zilizopo katika eneo la Carebien Pacific.

Zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo kame wanategemea kuendesha maishayaokwa kuvuna rasilimali zinazopatikana.

Lakini kuongezeka kwa idadi ya watu kumezusha wasiwasi mkubwa juu ya majaliwa na wananchi kwenye maeneoyaohivyo kuanzishwa kwa mpango huo kutasaidia kupunguza wasiwasi huo.