Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laongeza muda wa operesheni za EU CAR

UN Photo/Paulo Filgueiras
Baraza la Usalama. Picha:

Baraza la Usalama laongeza muda wa operesheni za EU CAR

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja wamepitisha azimio la kuongeza muda wa idhinisho lake kwa Muungano wa Ulaya kuendelea na operesheni zake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, chini ya azimio namba 2134 (2014), hadi tarehe 15 Machi 2015.

Katika mswada wa azimio hilo, Baraza la Usalama limesema kuwa limezingatia waraka wa Rais wa mpito wa CAR, Catherine Samba-Panza na ule wa Catherine Ashton, Mwakilishi Mkuu wa EU kwa rais wa Baraza hilo.

Azimio hilo, kwa mujibu wa mswada wake, pia limetokana na tathmini ya Baraza la Usalama kuwa hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati inaendelea kuwa tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.