Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka fedha zaidi ili kuwezesha kukabiliana na Ebola

Picha: UNICEF Sierra Leone/2014/Dunlop

Ban ataka fedha zaidi ili kuwezesha kukabiliana na Ebola

Katibu Mkuu Ban Ki-moon amekaribisha ahadi za kifedha ambazo zinatolewa na nchi mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya Ebola akisema ugonjwa huo ni tatizo la kimataifa linalohitaji juhudi za haraka kutokana na mahitaji ikiwamo  madkatari waliofunzwa na maabara.

Msemaji wa Bwana Ban, Stephan Dujarric amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa  Katibu Mkuu ameshukuru serikali za Australia, Colombia na Venezuela kwa amana za fedha na ahadi zinazofikia takribani dola milioni 14 na kupongeza serikali ya jamhuri ya Korea iliyoahidi leo dola milioni 5. Amesema hadi sasa ahadi zilizotolewa ni dola milioni 50 na kuonegeza kuwa fedha zaidi zinahitajika.

Kuhusu namna bora ya kupambana na Ebola msemaji wa Ban anasema.

(SAUTI DUJARRIC)

"Njia pekee ya kumaliza janga la Ebola ni kukomesha gonjwa hili la mlipuko kwa kuzingatia chanzo. Watu na serikali za Afrika Magharibi wanadhihirisha hatua muhimu. Dunia ina jukumu la kutoa msaada kwa kile ambacho nchi zimeomba."

Dujarric amesema mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ofisi ya umoja huo kuhusu dharura ya Ebola, UNMEER Anthony Banbury amewasili nchiniGuineaambapo atakutana na mamlaka mbalimbali akiwamo rais wan nchi hiyo ili kueleza mikakati ya UNMEER katika kukabiliana na janga hilo nchini Guinea.