Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatimaye watoto walioko Kobane wapatiwa misaada:UNICEF

Watoto wa Syria walio kwenye kambi za wakimbizi. (Picha:UM)

Hatimaye watoto walioko Kobane wapatiwa misaada:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa msaada aw vifaa vya kujisafi, maji na biskuti zenye virutubisho kwa maelfu ya watoto waliokimbia mapigano kwenye mji wa mpakani wa Kobane nchini Syria na kusaka hifadhi mjini Aleppo.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Syria, Hanna Singer amesema msaada huo ni mdogo lakini ni muhimu sana katika juhudi zao za kufikia watoto hao ambao ni miongoni mwa waaathiriwa wakubwa wa mapigano yanayoendelea akisema wanatumai kuona msaada zaidi wa aina hiyo kwingineko Syria katika wiki zijazo.

Christopher Boulierac ni msemaji wa UNICEF Geneva;

(Sauti ya Singer)

Timu yakujitolea kutoka kwa Shirika la hilal nyekundu la Syria hivi karibuni itaanza usambazaji wa vifaa katika kitongoji cha Afrin kilichoko Allepo ambapo kwa wastani  familia 1,000 kutoka Kobane wanaendelea kuishi.

Hata kabla ya kuanza kwa mapigano, mji wa Kobane haukuwa umepokea misaada kwa miezi 12.