Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa OCHA CAR aelezea wasi wasi wake kuhusu mauwaji

Wakimbizi wa CAR wanaokimbilia nhci jirani ya Chad.Picha ya UM/Emmanuelle Schneider

Mratibu wa OCHA CAR aelezea wasi wasi wake kuhusu mauwaji

Mratibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Claire Bourgeois, ameelezea wasi wasi wake mkubwa kuhusiana na kuuawa kwa watu wakati wa wimbi mpya la mashambulizi na vurugu mwanzonii mwa wiki hii.

OCHA imesema tangu Oktoba 14, zaidi ya  watu 159 waliojeruhiwa wamepokea matibabu ikiwa ni wiki moja tangu mgogoro kuzuka, huku zaidi ya watu 3,000 wakilazimika kukimbia makwao.

Halikadhalika, Bourgeois amepongeza hamasa na ujasiri wa wafanyakazi wa afya katika hospitali ambapo waliojeruhiwa wanapata huduma ya matibabu kwa  kufanya kazi usiku na mchana katika mazingira magumu.

Jens Laerke ni msemaji wa OCHA.

Takwimu za waliokimbia kwa ujumla zimeongezeka na kufikia watu 9500. Na wakati huu hatuwezi kusema ikiwa baadhi yao wamerudi makwao kwa sababu hali ya usalama imetuzuia kuhakiki mashinani. Mratibu wa masuala ya kibinadamu pia ameshutumu kushirikishwa kwa watoto katika mashambulizi baada ya mashirika ya kibinadamu kuripoti idadi kubwa ya watoto katika vituo vya upekuzi na vizuizi katika mji mkuu"