Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hayati Prof. Ali Mazrui, mchango wake katu hautosahaulika!

Hayati Profesa Ali Mazrui, siku ya uzinduzi wa kitabu cha Mwalimu Nyerere kwenye Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Idhaa ya Kiswahili)

Hayati Prof. Ali Mazrui, mchango wake katu hautosahaulika!

Usiku wa tarehe 12 Oktoba 2014, mjini New York, mwanamajumui, msomi, mwalimu na mwanafasisi nguli wa Afrika kutoka Kenya, Profesa Ali Mazrui aliaga dunia!

Hayati Profesa Mazrui alizaliwa Mombasa Kenya mwaka 1933 na hadi umauti unamkuta alikuwa Mkurugenzi wa kitivo cha masomo ya kitamaduni ulimwenguni kwenye chuo kikuu cha Binghamton, jijini New York, Marekani.

Nguli huyu aligusa maisha ya wengi, alipita sehemu nyingi na alama alizoacha ndizo Assumpta Massoi amekukusanyia na ungana naye basi kwenye makala hii ya wiki.