Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati dhidi ya Ebola, WFP yaimarisha usaidizi wa kiufundi

WFP inatoa mgao wa chakula katika maeneo yaliyoathirika na ebola.Picha@WFP

Harakati dhidi ya Ebola, WFP yaimarisha usaidizi wa kiufundi

Wakati Umoja wa Mataifa ukiendelea kusihi wadau kusaidia harakati dhidi ya mlipuko wa Ebola huko Afrika Magharibi, Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, limesambaza misaada ya kiufundi- hususan kwa wadau wa afya nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Misaada hiyo ni pamoja na uagizaji wa vifaa vinavyotakiwa ikiwemo magari ya wagonjwa na majengo ya kuhifadhi maiti.

Mathalani imesaidia Sierra Leone ununuzi wa magari 74 ya wagonjwa na malori ya kusambaza vifaa ambapo magari 30 kati ya hayo yanawasili Jumamosi.

Vifaa hivyo vitasafirishwa kwa ndege kuelekea maeneo ya ndani zaidi ili kuwezesha harakati dhidi ya Ebola wakati huu ambapo WFP tayari imeshatoa usaidizi wa chakula kwa wananchi walioathirika kwa Ebola.

Msemaji wa WFP Geneva, Uswisi, Elizabeth Byrs amesema nchini Guinea wanasaidia vifaa vya mawasiliano.

(Sauti ya Byrs)

Nchini Guinea WFP itapeleka vifaa vya mawasiliano ili kuwezesha huduma ya upashanaji taarifa ya kijamii na pia kuwezesha wanafamilia kuwasiliana na wale waliopo kwenye vituo vya tiba dhidi ya Ebola.”