Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani kuuwawa kwa walinda amani watatu wa Darfur

UN Photo - Jean-Marc Ferre
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Picha:

Ban alaani kuuwawa kwa walinda amani watatu wa Darfur

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amelaani mauaji ya walinda amani watatu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika Darfur, UNAMID ambao wameuwa kaskazini mwa jimbo hilo baada ya watu wasiojulikana waliojiahami kwa silaha kuwavamia.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu Ban akisema askari wawili kati yao walikufa papo hapo huku mwingine akijeruhiwa vibaya ambapo hata hivyo alipoteza maisha baadaye.

Taarifa hiyo inasema shamabulio hilo la ghafla dhidi ya walinda amani hao raia wa Ethiopia lilitokea wakati wa doria ambapo walikuwa wakilinda katika kisima cha maji.

Ban amesisitiza kuwa mashambulizi kama hayo kwa walinda amani hayakubaliki na ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu na serikali ya Ethiopia.

Kuuwawa kwa walinda amani hao watatu wanafikisha idadi ya walinda aamni 61 waliouwawa tangu kuanzishwa kwa ujumbe wa kulinda amani UNAMIDI mwezi December, 2007