Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya Kuelekea Mkataba mpya kuhusu tabianchi yaanza Bonn

Mazungumzo ya Kuelekea Mkataba mpya kuhusu tabianchi yaanza Bonn

Duru ya mwisho ya mazungumzo rasmi kabla ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa Tabianchi utakaofanyika huko Peru, utaanza wiki kesho mjini Bonn Ujerumani.

Mkutano huo utakaofanyika kati ya tarehe 20-25, utatoa fursa muhimu zaidi kwa serikali kuboresha nakala ya rasimu mpya ya makubaliano ya tabianchi.

Katika taarifa, kamati ya Umoja wa Mataifa ya mkataba kuhusu makubaliano ya tabianchi, UNFCCC, imesema wakati wa kipindi cha mwaka wa 2015, rasimu hiyo itakuwa msingi wa mazungumzo mapya kuhusu makubaliano ya mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika mjini Paris, Ufaransa mwakani.

Halikadhalkika, kama sehemu ya hili, serikali itaupata uelewa wa ndani kuhusiana na nini kila nchi itachangia katika kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi.