Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama wa chakula ni muarubaini wa maendeleo endelevu vijijini: IFAD

UN Photo/Evan Schneider
Rais wa mfuko wa maendeleo ya kilimo duniani IFAD Kanayo Nwanze.

Usalama wa chakula ni muarubaini wa maendeleo endelevu vijijini: IFAD

Rais wa mfuko wa maendeleo ya kilimo duniani IFAD Kanayo Nwanze amesema hakuna maendeleo endelevu ikiwa hakuna usalama wa lishe na chakula kwa watu wa vijijini.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Bwana Nwanze amesema ni lazima kuimarisha uwekezaji vijijini ili kuwakomboa raia waioshio maeneo hayo katika umaskini akisisitiza

(SAUTI)

"Wazalishaji,wakulima, wavuvi na wafugaji wadogowadogo huzalisha karibu asilimia 80 ya chakula katika nchi zinazoendelea. Lakini cha kushangaza watu hawa wanaishia kulala njaa. Hii sio hali endelevu ikiwa ni kwa vitendo au nadharia na hakuna tija kwa maendeleo enedelevu ikiwa wataachwa."

Amesema ujumuishwaji katiaka maendeleo ya kilimo ni uwekaji wa sera bora na uchumi na kuongea kuwa ikiwa uwekezaji wa kweli utaelekezwa vijijini, usalama wa chakula na lishe utaimarishwa na kuwa na jamii imara