Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani na haki za watoto vyamulikwa Darfur

Mkuu wa kikosi cha UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella. (Picha:Sojoud Elgarrai UNAMID).

Amani na haki za watoto vyamulikwa Darfur

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika katika Darfur UNAMID umekaribisha mpango mkakati wa kijamii wa kusitisha utumiwaji wa watoto katika mapigano baina ya koo jimboni humo.

Mpango huo ulioasisiwa na Sheikh Musa Hilal na kuidhinishwa na wazee wa makabila Kaskazini mwa Darfur, umepongezwa na UNAMID ukielezwa kuwa ni hatua muhimu katika kulinda haki za watoto.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa mchakato wa amani jimboni humo unakwamishwa na baadhi ya makundi yanayopigana ambayo hayajasaini makubaliano ya kuleta amani ya Doha (DDPD), amesema mkuu wa kikosi cha UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella.

(SAUTI MELLA)

Hata hivyo kamanda Mella amesema UNAMID umefanya juhudi mara kadhaa ambapo kuna matumaini ya kujumuisha makundi haya katika makubaliano lakini kikwazo ni

(SAUTI MELLA)