Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kay alaani shambulizi la bomu Mogadishu

Mwakili maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay.Picha ya UM/Jean-Marc Ferré

Kay alaani shambulizi la bomu Mogadishu

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja nchini Somalia, Nicholas Kay, amelaani shambulizi la bomu la kutumia gari lililofanyika jana usiku mjini Mogadishu, na ambalo lilisababisha vifo na majeraha kwa watu wengi.

Kwa mujibu wa Rais wa Somalia, watu wapatao 13 waliuawa. Kay amelaani shambulizi hilo la kigaidi lililolenga raia wasio na hatia, akisema kuwa vitendo kama hivyo dhidi ya raia wa ukatili usiokubalika.

Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu amewapongeza walinzi na wahudumu wa afya kwa kuchukua hatua haraka, huku akitaka watekelezaji wa kitendo hicho kuchukuliwa hatua za kisheria haraka.

Aidha, Bwana Kay amesema wanasimama kidete katika msaada wao kwa raia wa Somalia katika juhudi zao za kuwa na amani na utulivu katika siku zijazo.