Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atoa wito kuhusu siku ya majanga duniani

Katibu Mkuu Ban Ki-moon.Picha ya UM/NICA

Ban atoa wito kuhusu siku ya majanga duniani

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya majanga ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 13, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kuwajali watu wazee akisema kuwa mara nyingi hali ya dharura inapotokezea basi watu wa kundi hilo wapo hatarini zaidi. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Sauti ya George)

Katika taarifa yake kuadhimisha Siku ya Majanga Duniani Ban ameonyesha wasiwasi wake kuhusiana na dunia inavyowajali watu wenye umri mkubwa zadi na kusema kwamba uzoefu umeonyesha kwamba watu wa kundi hilo ndiyo waathirika wakubwa pindi majanga yanapojitokeza.

Alisema kuwa hesabu za hivi sasa zinaonyesha kwamba wakati dunia ikiwa na jumla ya watu wanasadikika kufikia milioni 700 huku asilimia kumi ya watu hao ni watu wazee wanaozidi umri wa miaka 60.

Amesema kuwa kulingana na mwenendo wa mambo ulivyo hivi sasa kuna uwezekano mkubwa ifikapo mwaka 2030 dunia ikawa na idadi kubwa ya watu wazee kuliko watoto jambo ambalo litakuwa limejitokeza kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia.

Amesema kuwa kwa kuziangalia takwimu hizo kuna haja sasa ya kutambua mchango unaotolewa na watu wazima ikiwamo wazee hasa pale kunapojitokeza majanga ya aina mbalimbali.