Ban kutembelea kambi za wakimbizi Gaza

13 Oktoba 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametangaza kuwa atatembelea ukanda wa Gaza, jumanne tarehe 14, Oktoba.

Amesema hivo akiongea na waandishi wa habari mjini Cairo, nchini Misri, baada ya mkutano wa kimataifa wa ngazi ya juu kuhusu ukarabati wa Gaza.

Kwa mujibu wa Chris Gunness, msemaji wa Umoja wa Mataifa katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuhudumia wakimbizi wa Palestina, UNRWA , Ban atetembelea kambi ya wakimbizi wa ndani, wakati bado watu 50,000 wametafuta hifadhi kwenye kambi za UNRWA. Atatembelea pia shule iliyobomlewa na makomboro na mradi wa kuendeleza wavuvi.

Akiongea na redio ya Umoja wa Mataifa Chris Gunness amesema siyo mara ya kwanza kwa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuenda kwenye ukanda wa Gaza, katibu mkuu amewahi kuonyesha huruma sana kwa hatma ya wapalestina.

Gunness amesema ziara hi itakuwa fursa kwa Ban ya kurudia wito wake kwa suluhu ya kisiasa.

«  Amesema, hakutakuwa tena ukarabati wa Gaza. Na nadhani kwamba ni wazi kuwa katibu Mkuu anataka ujumbe wa kisiasa wa moja kwa moja, ujumbe wa usalama, kwamba hatuwezi kujenga tena Gaza upya na kubomolewa tena. Tunapaswa kujionda na mwelekeo huu wa kuzingirwa, kurusha maroketi nz kisha makonbora »

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter