Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ebola imebadili mwelekeo wa shughuli zetu Liberia: UNMIL

Meja Jenerali Ngondi (kushoto). Picha: UNMIL

Ebola imebadili mwelekeo wa shughuli zetu Liberia: UNMIL

Nchini Liberia, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu mwezi Machi mwaka huu umelazimisha kubadilika kwa mwelekeo wa shughuli za ujenzi wa nchi hiyo iliyokuwa inaanza kuibuka baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake nchini humo UNMIL nao pia umelazimika kubadili mwelekeo angalau kwa muda kwani Ebola inatishia siyo tu afya ya jamii bali pia usalama.

Je hali ikoje? Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza na Kamanda Mkuu wa vikosi vya UNMIL, Meja Jenerali Leonard Ngondi, ambaye hapa anaanza kwa kuelezea hali ilivyo kwa sasa.