Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fikra za Mahatma Gandhi zina nafasi kubwa sasa kuliko wakati wowote

UN Photo/Jennifer S Altman
Tukio la kumuenzi Mahatma Gandhi.

Fikra za Mahatma Gandhi zina nafasi kubwa sasa kuliko wakati wowote

Miaka 66 iliyopita, baba wa Taifa la India, Mahatma Gandhi aliuawa. Hata hivyo hadi hii sasa fikra na falsafa zake zimeendelea kupigiwa chepuo ikizingatiwa mazingira ya sasa ya mizozo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ni kwa misingi hiyo, ujumbe wa kudumu wa India kwenye Umoja wa Mataifa uliandaa tukio maalum likienda sambamba na siku ya kuzaliwa kwake tarehe Pili Oktoba, ambayo hutambuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni siku ya kupinga ghasia. Kufahamu yaliyojiri ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.