Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaweka viwango wastani vya kuboresha mifumo ya kutunza misitu

Picha: FAO/Joan Manuel Ballielas

FAO yaweka viwango wastani vya kuboresha mifumo ya kutunza misitu

Shirika la Kilimo na Chakula, FAO, limezindua vyombo vya bure ambavyo linatarajia kuwa vitaboresha jinsi nchi zinazoendelea zinavyofuatilia hali ya misitu yao ili kukabiliana na uharibifu wa misitu na mabadiliko ya tabianchi.

Serikali za Finland na Ujerumani zimesaidia katika kuunda chombo kiitwacho Open Foris, ili kuzisaidia nchi katika uwekaji daftari zote za misitu, kuanzia kukagua, kuandaa na kukusanya takwimu hadi kutathmini na kuripoti. FAO inasema kuwa habari kamili kuhusu misitu ni muhimu kwa kuwezesha serikali kudhibiti rasilimali zao za asili kwa njia endelevu, lakini takriban asilimia 80 ya nchi zinazoendelea zinapata ugumu kupata na kutumia habari za msingi kuhusu rasilimali zao za misitu.

Halikadhalika, FAO imesema kuwa ukataji miti na uharibifu wa ubora wa misitu unaotendeka hususan katika nchi zinazoendela, ni miongoni mwa vyanzo vikubwa zaidi vya hewa chafuzi ya ukaa au kaboni inayozalishwa kote duniani na vitendo vya wanadamu.