Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya afya ya akili: dhiki yaangaziwa

Mwanamke akisimama mbele ya graffiti ya jua inayowakilisha maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani. Picha: UN / M. Perret

Siku ya afya ya akili: dhiki yaangaziwa

Leo ni siku ya kimataifa ya afya  ya akili , ikiwa na dhamira ya kuendeleza uelewa kuhusu masuala ya afya ya akili duniani, na kuchagiza juhudi za kusaidia huduma za afya ya akili.

Kauli mbiu ya mwaka huu wa 2014 ni “Kuishi na dhiki”, na Shirika la Afya Duniani linamulika jinsi watu wanavyoweza kuishi kwa afya hata ikiwa wamekumbwa na tatizo la dhiki, au schizophrenia katika Kiingereza.

Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa hii Daktari wa magonjwa ya akili kutoka Tanzania Patrick Elias anasema uelewa kuhusu magonjwa ya afaya ya akili ni muhimu katika kupambana na maradhi hayo.

(SAUTI PATRICK)